SUBIRI NIKUPE SIRI.
Subiri nikupe siri, ilonileta mjini.
Nilingia mjini, si mdogo akilini.
Nilifikia Masaki, ni maarufu jijini.
Langu mimi ni dhumuni, kwenda Tambaza Shuleni.
Subiri nikupe siri, toka nifike mjini.
Usitoe majisifu, kwa kusifia mjini.
Cha ajabu sikioni, ni bora ya kijijini.
Maradhi yao sukari, kwa kupanda mwendo kasi.
Posta na Gerezani, eti kwao ndio mbaali.
Subiri nikupe siri, toka nifike mjini.
Hakuna shamba mjini, labla nikalime lami.
Mmejazana mtoni, kwenye Mto Msimbazi.
Wangu mimi utafiti, maji asili ni nini.
Ukijuwa ya mjini, hutokula abadani.
Subiri nikupe siri, toka nifike mjini.
Hujifanya ni wasomi, na kubishana kihuni.
Wanachanganya mjini, kilo rasmi kiswahili.
Lugha kwao mtihani, kichina huwa mwishoni.
Ni bora wa vijijini, tunalinda tamaduni.
Subiri nikupe siri, toka nifike mjini.
Daima nnathamini, mimi kwetu kijijini.
Kila muda nasafiri, kurudi kwetu nyumbani.
Kuwasabahi wazazi, na yule wangu ayuni.
Kama kweli huamini, nifate pale stendi.
Subiri nikupe siri, toka nifike mjini.
© Zanzibar Poems
0 Comments:
Post a Comment